Micheweni FM
Micheweni FM
16 November 2026, 1:52 pm

katika bonanza la amani na mshikamano lililofanyika katika uwanja wa Pwepweu, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Na Essau Kalukubila.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Khatib Juma Mjaja, amewataka wananchi wa Tumbe kuendelea kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, akieleza kuwa hali hiyo ndiyo msingi wa maendeleo na ukuaji wa uchumi wa wananchi pasipo kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa shehia za Tumbe Mashariki na Tumbe Magharibi katika bonanza la amani na mshikamano lililofanyika katika uwanja wa Pwepweu, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba
Amesema pamoja na wananchi wengi kutambua umuhimu wa amani na mshikamano, bado ipo haja ya kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii ili kuongeza uelewa na ushiriki katika kudumisha misingi hiyo muhimu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa NCA, Eva Knutsen, amesema mradi huo wa kuhamasisha amani na mshikamano kupitia dini mbalimbali unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na serikali ili kudumisha amani na utulivu. Aidha, amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ili kuwezesha maendeleo ya serikali na jamii kufikiwa kwa ufanisi.
Bonanza hilo limeandaliwa na Taasisi ya Norwegian Church Aid (NCA) kupitia Mradi wa Swahili Coast, unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Pemba kwa lengo la kuziunganisha jamii na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kijamii.