Micheweni FM

CCM Kaskazini Pemba wakabidhiana ofisi

6 October 2026, 4:22 pm

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskzini Pemba Salum Khamis Haji akiingia katika Ofisi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Picha na Essau alukubila.

Hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa kasikazini pemba yaliofanyika Oktoba 5. 2026

Na Masanja Mabula

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salum Khamis Haji, amekabidhiwa rasmi ofisi hiyo, na kuahidi kuimarisha utendaji kwa kushirikiana na viongozi wa chama na Serikali, ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Katibu Salum amesema atashirikiana kwa karibu na viongozi wa Serikali katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ili wananchi waone matokeo chanya na kuendelea kuwa na imani na juhudi za maendeleo zinazotekelezwa.

Sauti ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba

Nao Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba wameahidi kumpa ushirikiano Katibu huyo, ili kuongeza ufanisi wa majukumu na kusimamia mipango ya chama.

Uongozi wa Salum Khamis Haji unaanza kwa ahadi ya ushirikiano na utendaji wenye kuzingatia maendeleo, huku matarajio yakiwa ni kuona juhudi hizo zikizaa matokeo chanya na manufaa zaidi kwa wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.