Micheweni FM

Watendaji wa Halmashauri Micheweni watakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato

4 November 2026, 8:35 am

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi, , Mheshimiwa Abdulwahab Said Abubakari akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Micheweni hawapo pichani ,(picha na Mwiaba Kombo)

Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni wametakiwa kubuni na kuibua vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuiwezesha halmashauri hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Na Mwiaba Kombo

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri hiyo Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mheshimiwa Abdulwahab Said Abubakari,amesema Micheweni ya sasa imebadilika ikilinganishwa na ilivyokuwa hapo awali, hivyo kuna haja ya halmashauri hiyo kujipambanua kwa kubuni mbinu na mikakati mipya ya kuongeza mapato ili kwenda sambamba na mahitaji ya maendeleo ya wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi,mheshimiwa Abdulwahab Said Abubakar

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mikidadi Mbarouk Mzee, amemuahidi mwenyekiti huyo kuwa ofisi yake itafanya mabadiliko mbalimbali yatakayosaidia kuboresha utendaji kazi, ikiwemo kuandaa mafunzo kwa watendaji wa halmashauri hiyo.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mikidadi Mbarouk Mzee

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Hamad Khatib Saleh, amemhakikishia mwenyekiti huyo kuwa ushauri na maelekezo yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha halmashauri hiyo inaimarisha ukusanyaji wa mapato na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi huku mhasibu wa mapato wa halmashauri hiyo, Mchanga Faki Ali, amesema ofisi yake itaendelea kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato vilivyopo pamoja na kubaini fursa mpya zitakazosaidia kuongeza mapato na kuimarisha uwezo wa kifedha wa halmashauri hiyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Micheweni Hamad Khatib Saleh ,sauti ya mhasibu mapato wa halamashauri Mchanga Faki Ali