Micheweni FM
Micheweni FM
29 September 2026, 12:45 pm

Mbunge wa Jimbo la Micheweni atimiza ahadi yake kwa Jumuiya ya Bodaboda ya Jimbo hilo, baada ya kutoa hadi hiyo ya kuwasaidia vijana kuwainua kiuchumi kupitia ukimbizaji Bodaboda
Na Essau Kalukubila.
Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Mahesh Shah Bolisha, amekabidhi pikipiki kwa vijana wa jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha kiuchumi na kuwasaidia kuongeza kipato kupitia shughuli za usafirishaji.
Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo wakati wa hafla ya makabidhiano, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Amina Ali Haji, amesema mpango huo unalenga kuwawezesha vijana kujiajiri, kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Jimbo la Micheweni, Salimu Jabu Khamis, amesema utoaji wa pikipiki hizo unaonesha namna mbunge huyo anavyotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo kupitia miradi inayogusa maisha ya wananchi.
Kwa upande wao, Mwenyekiti wa Bodaboda pamoja na mmoja wa wanachama wa bodaboda katika jimbo hilo wamesema kitendo hicho kimeweka historia Micheweni kwani msaada wa aina hiyo haujawahi kutolewa hapo awali.
Wanufaika wa pikipiki hizo wameahidi kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujiongezea kipato, kukidhi mahitaji ya familia zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Jimbo la Micheweni.