Micheweni FM
Micheweni FM
22 October 2026, 12:29 pm

Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, Waziri Haroun amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta zilizopewa kipaumbele katika maboresho hayo
Na Masanja Mabula.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, amesema ongezeko la mishahara lililofanywa na Serikali linalenga kutambua na kuthamini mchango wa watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, Waziri Haroun amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta zilizopewa kipaumbele katika maboresho hayo
Aidha ameitaja sekta ya Afya kwamba nayo imeguswa na maboresho hayo ya Mishahara mipya ambayo inatarajia kulipwa mwezi huu
Ameongeza kuwa ongezeko hilo ni la mara ya tatu kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nane, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha maslahi ya watumishi wa umm
Waziri Haroun amesema serikali itaendelea kuimarisha maslahi ya watumishi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.