Micheweni FM

Wahitimu ualimu CCK Pemba watakiwa kujiendeleza

20 September 2023, 7:18 am

Baadhi ya wahitimu wa ualimu chuo cha kiislam Pemba wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi wengine walihudhudhuria kwenye mahafali ya pili ya chuo hicho (picha na Mwiaba Kombo)

Chuo cha kiislam Pemba ni miongoni mwa chuo ambacho kipo kisiwani Pemba ambapo kinatoa fani ya ualimu kwa ngazi ya cheti na diploma

Na Mwiaba Kombo

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais tawala za Mikoa ,Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ mh Masoud Ali Mohammed amewahakikishia walimu ,wanafunzi pamoja na wanachi kuwa zitafanyiwa kazi changamoto zote zilizoelezwa katika mahafali ya pili ya chuo cha kiislam Pemba .

Akisoma hotuba kwa niaba ya waziri huyo mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mh Salama Mbarouk Khatib amesema zipo changamoto nyingi ambazo zimeelezwa hivo ni jukumu la serikali kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto hizo .

Amesema kazi za viongozi wa serikali ni kuhakikisha wanawasimamia wananchi na kuweza kuwatatulia changamoto zao ambazo zinawakali katika maeneo yao.

Nae mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amewataka wahitimu hao kuendelea kujitaftia elimu kwani hapo sio mwisho wao.

Amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanajiendeleza kielimu kwani elimu haina mwisho hivo ni jukumu lao kuhaikisha wanaendeleza elimu yao.

Kwa upande wake afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya Amali  Pemba Mohammed Nassor Salim amewataka wahitimu hao kuendelea kujitolea kusomesha kwani kwasasa serikali imeandaa bajeti kubwa kwa ajili ya ajira mpya.

Mkurugenzi wa idara ya mafunzo ya ualimu Zanzibar Rashid Abdul aziz Muki amesema hili jambo chuo cha kiislam lisitudogoshe na kuacha kuwapeleka wanafunzi kujipatia elimu katika chuo hicho.

 Mkuu wa chuo hicho Mkasha Sharif amewataka viongozi hao kuhakikisha  juhudi Zaidi zinafanyika kwani  kuna upungufu mkubwa kwa skuli za sekondari.

Mahafali hayo ni ya pili katika chuo hicho ambapo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali pamoja na wananchi.