Micheweni FM

Wanafunzi Pemba watakiwa kujiunga na IIT Madrasa

7 March 2024, 12:36 pm

Afisa uhusiano kutoka taasisi ya Chuo kikuu cha  Tecknolojia cha India tawi la Zanzibar Mwatima Rashid Issa akizungumza na wanafunzi.

IIT Madrasa ni chuo kikuu chenye kujitegemea kinachotoa kozi mbali mbali za Teknolojia ambapo ujio wake hapa hapa Zanzibar kitaweza kutangaza fursa nyingi na kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa ya maendeleo kwa upande wa Zanzibar.

Na Mwiaba Kombo

WANAFUNZI kisiwani Pemba wametakiwa kujiunga taasisi ya Chuo kikuu cha  Tecknolojia cha India tawi la Zanzibar (IIT Madrasa in Zanzibar)ili kuweza kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa ya maendeleo ya nchi na watu wake kielimu na jamii kwa ujumla .

Hayo yameelezwa na Afisa uhusiano kutoka chuo hicho Mwatima Rashid Issa wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita katika Skuli ya Sekondar Madungu chake chake Pemba

Amesema lengo la kuja kisiwani Pemba ni kuendelea kukitangaza chuo hicho na kuweza kukitambua na kutambua fursa mbali mbali mbali ambazo zinapatikana chuoni hapo na baada ya kumaliza masomo yao waweze kujiunga na chuo hicho.

Mwatima amewataka wanafunzi hao kuchangamkia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia pia kuwatoa hofu wale wote ambao wanataka kujiunga na chuo hicho.

Kwa upande wao wanafunzi ambao wamepatiwa mafunzo hayo wamesema ujio wa chuo hicho utawasaidia kusoma fani tofauti tofauti ambazo zitaweza kuwasaidia katika harakati zao za maisha baada ya kumaliza masomo yao .

Wamsema kupitia chuo cha IIT Madrsa watapata fursa nyingi ambazo zitaweza wasaidia na kuacha kutegemea ajira kutoka serikalini kwasababu ukimaliza chuo hicho unaweza kujiajiri mwenyewe .

Aidha wamewataka wanafunzi wengine ambao wanamaliza masomo yao kuhakikisha wanajiunga na chuo hicho ambacho fursa nyingi zinapatikana chuoni hapo.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha wanafunzi tofauti tofauti kutoka mkoa wa kusini Pemba ambazo ni Skuli ya Madungu Sekondari ,Fidel Castrona Mohd Juma Pindua.