Micheweni FM

RC Kusini Pemba: Lipeni kodi kwa maendeleo ya nchi

25 November 2023, 6:31 pm

Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali akizungunmza na wananchi ,wafanyakazi wa taasisi mbali mbali ikiwa ni wiki ya shukrani kwa walipa kodi kutoka TRA (picha na Mwiaba Kombo)

Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) ni shirika la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo lina wajibu wa kusimamia na kukusanya na kuhifadhi mapato yote kama ambavyo sheria zinasema na ni kwa niaba ya Serikali.

Na Mwiaba Kombo

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud amewataka wananchi kuendelea kuiunga na kushirikiana na serikali kwa kulipa kodi zao ili ziweze kutumika katika kuwaletea maendeleo.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali huko Gombani Chake Chake alipokuwa  akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya shukrani kwa mlipo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Amesema kuwa  kodi zinazotolewa na wananchi hao ndizo ambazo zinatumika kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi hao,hivo ni vyema kuhakikisha wanaendelea kulipa kodi.

Kwa upande kaimu meneja TRA mkoa kikodi Pemba Nuhu mohd Suleiman amesema kila inapofika mwezi wa November wanaandaa wiki ya shukrani kwa walipa kodi.

Akitoa neno la shukrani meneja msaidizi forodha Pemba Suleiman Abdalla Said amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na TRA katika suala zima la kulipa kodi.

Wiki ya mlipa kodi Pemba imeanza na matembezi maalum ambayo yalianzia viwanja vya tibirinzi na kumalizia viwanja vya Gombani ambapo wananchi ,wafanyakazi kutoka taasisi mbali mbali pamoja na wanavikundi vya mazoezi walishiriki katika maandamano hayo ambayo yaliongozwa na mkuu wa wilaya ya Chake chake .