Micheweni FM

Mkaguzi wa polisi jamii amwaga vifaa kwa wanafunzi wanaojitayarisha na mitihani

8 August 2023, 11:51 am

 Inspector Khalfan akimkabidhi taa mwanafuzi wa skuli ya pandani kwa ajili ya matumizi ya kusomea (picha na Essau Kalukubila)

Wanafunzi wa skuli za Pandani msingi na sekondari wakipokea vifaa ambavyo vitawasaidia kwa ajili ya kujisome baada

Na Essau Kalukubila

Wanafunzi wa skuli ya msingi na sekondari Pandani pamoja na sekondari Wete ambao wanajitayarisha na mitihani yao ya taifa, wamepatiwa msaada wa tochi na balbu vyenye thamani ya shilingi 23,5000 kwa ajili ya kuwasaidia wakati umeme unapozimwa.

Msaada huo umetolewa na Mkaguzi wa Polisi jamii shehia ya Pandani, Inspector Khalfan Ali Ussi baada kutembelea kambi ya wanafunzi hao na kuona hali halisi ilivyo wakati unapozima umeme, jambo ambalo linawapa usumbufu wakati wanapopitia masomo yao.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo ameeleza kuwa, vitaweza kuwasaidia wanafunzi hao katika kujisomea wakati umeme unapokata kwenye mabweni yao.

Inspector Khalfan amewataka wanafunzi hao kujitahidi katika masomo yao, ili waweze  kufaulu vizuri na kuwa wakombozi katika familia zao na taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo Inspekta huyo amewasisitiza wanafunzi hao kuacha rushwa muhali kwani inarudisha nyuma maendeleo yao na jamii kwa ujumla. 

Mapema Mratibu wa Polisi Jamii Mkoa wa Kaskazini Pemba Inspekta Makame Ali Makame amefahamisha kuwa, lengo la kuanzishwa Polisi jamii nchini, ni kuhakikisha wanaondosha vitendo vya uhalifu ambavyo vimekithiri katika jamii.

Nae Kaimu mwalimu Mkuu wa skuli ya msingi Pandani Halima Khalifan Said aliupongeza uongozi wa Polisi jamii hehia ya Pandani kwa kuwapatia wanafunzi hao msaada, ambapo umewapa faraja na furaha.

Nae mwanafunzi Fatma Salim alitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake na kusema kuwa kutatuliwa changamoto hiyo iliyokuwa ikiwakabili, imewapa matumaini makubwa kuendelelea na masomo yao.