Micheweni FM
Micheweni FM
22 October 2026, 11:54 am

Baadhi ya wanufaika wa Mradi huo wamesema Mradi umeimarisha uchumi wao baada ya kupata mafunzo ya kuzalisha na kusarifu bidhaa zinazotokana na rasilimali za bahari
Na Essau Kalukubila.
MRADI wa INCLU-CITIES unaojishughulisha na rasilimali za baharini unaosimamiwa na ENABU kupitia vyuo vya Amali chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya EU unatajwa kuwa nguzo muhimu kwa wananchi wamaeneo yaliyozungukwa na bahari katika kuchochea maendeleo na kutoa fursa za kiuchumi.
Baadhi ya wanufaika wa Mradi huo wamesema Mradi umeimarisha uchumi wao baada ya kupata mafunzo ya kuzalisha na kusarifu bidhaa zinazotokana na rasilimali za bahari Wamesema kabla mradi huo walikuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na kutokuelewa namna ya kuzitumia rasilimali za bahari ambapo kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa hali inayochangia kuendesha familia zao kupitia mradi huo.
Msimamizi wa Mradi huo Abuubakari Khatib amesema mradi huo unalenga kuwainua vijana na kuongeza thamani ya bidhaa za mazao ya baharini wanazozalisha.