Micheweni FM
Micheweni FM
27 September 2026, 7:44 pm

TCRA yatoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Micheweni yenye lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi salama ya simu ili kujikinga na utapeli mtandaoni.
Na Essau Kalukubila.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA imetoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kuhusu matumizi sahihi na salama ya simu za mkononi ili kujikinga na uhalifu wa mtandaoni.
Akiotoa elimu hiyo Othuman Bakari afisa kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Ofisi ya Zanzibar amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kutunzaji wa namba za siri, kuepuka kutoa taarifa binafsi kwa watu wasiowafahamu pamoja na namna ya kutambua ujumbe na simu za utapeli.
Sambamba na hayo Sheha wa Shehia ya Mapofu Assa Sharif Khalid na sheha wa Mjanaza Hamad Said Ali wamesema elimu iliotolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA itasidia kupunguza utapeli katika maeneo yao hali ambayo ilikuwa inawafanya wannchi kushuka kiuchumi wanapo tapeliwa
Nao Baadhi ya wananchi waliopa elimu hiyo wameishukuru Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa elimu hiyo ambayo itawasaidia kutambua mbinu zinazotumiwa na wahalifu wa mtandao kwa kuepuka kutapeliwa
TCRA imesema itaendelea kutoa elimu kama hiyo katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuimarisha usalama wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano.