Micheweni FM
Micheweni FM
12 October 2026, 11:47 am

Kwa miaka mingi kazi ya ufugaji wa Nyuki imekua ni kazi ya uvumilivu na maumivu na kuhatarisha maisha ambapo wafanyaji wa kazi hiyo wanakumbana na kadhia kadhaa ikiwemo kutafunwa na nyuki pindi wanapovuna asali huku wakiambulia uzalishaji duni wa asali usiokidhi mahitaji .
Na Masanja Mabula.
Baadhi ya wakulima wa Nyuki kisiwani pemba wameanza kupatiwa mafunzo kwa vitendo wakiwa shambani juu ya namna bora ya ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa ambayo sasa italeta tija kwa wafugaji na kuinua kipato .
Wafugaji hao wameeleza kua hatua hio ya kupewa taaluma kwa vitendo namna ya njia sahihi na bora za ufugaji wa Nyuki kutawaengezea ujuzi ambao u natoa fursa za kujiajiri na kuingiza kipato.
Kwa upande wake Afisa nyuki idara ya misitu Zanzibar Jokha Mtoro amesema idara imeamua kuwapatia wakulima wa Nyuki mafunzo hayo kwa vitendo ili kutambua namna bora ya ufugaji na uhudumiaji ili kupata asali na mazao bora yanayotokana na Nyuki ikiwa ni pamoja na upakaji wa Nta katika mzinga,utundikaji wa mizinga katika miti na machaga.
Sauti ya afisa Nyuki idara ya misiti Zanzibar Jokha Mtoro