Micheweni FM

Mkono kwa Mkono yawafikia wengi Kaskazini Pemba.

22 October 2026, 5:43 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya akizungumza katika mkutano wa mkono kwa mkono Picha na Essau Kalukubila.

viongozi wa sekta mbalimbali Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya taasisi zao pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo

Na Masanja Mabula.

Programu ya Mkono kwa Mkono inayoendeshwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) imeendelea kuwa chachu muhimu kwa taasisi katika kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa wakati na kuhakikisha taarifa zinawafikia walengwa.

Kampeni hiyo leo imewakutanisha viongozi wa sekta mbalimbali Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakitumia fursa hiyo kueleza mafanikio ya taasisi zao pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, ameitaka jamii kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño huku akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kujikinga ili kulinda maisha na mali zao.

Sauti ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Khamis Abdalla ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu, hususan katika kuwajengea wanafunzi ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kukabiliana na changamoto za maisha na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Khamis Abdalla

Nao baadhi ya viongozi walioshiriki katika hafla hiyo wamesema kampeni ya Mkono kwa Mkono imekuwa jukwaa muhimu la kuimarisha mawasiliano kati ya taasisi na wananchi, kwa kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu huduma na fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali.

Sauti ya baadhi ya viongozi walioshiriki katika hafla hiyo wamesema kampeni ya Mkono kwa Mkono

Wamesema ushirikiano kati ya ZBC na taasisi hizo ni muhimu katika kuendeleza utoaji wa elimu kwa umma na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa zinazowasaidia kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao ya kila siku.