Micheweni FM

RC Kaskazini Pemba ataka ushirikiano zaidi Bandari ya Wete

3 October 2026, 1:54 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya akizungumza katika kizi kilisho washirikisha maafisa mbalimbali wa bandari ya Bandari ya Wete katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete. picha na Essau Kalukubila

Kikao kazi cha kuboresha utendaji kazi, uendeshaji na uwajibikaji wa Bandari ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, kilichowashirikisha

Na Mwamizi Mohamed

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo katika kikao kazi cha kuboresha utendaji kazi, uendeshaji na uwajibikaji wa Bandari ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, kilichowashirikisha maafisa mbalimbali wa bandari katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete.

Amesema ushirikiano miongoni mwa watendaji wa bandari ni muhimu katika kusimamia shughuli za uingizaji na utoaji wa bidhaa, akibainisha kuwa kutokuwepo kwa mshikamano kunaweza kutoa mwanya kwa wafanyabiashara kutumia bandari bubu kupitisha bidhaa bila kufuata taratibu zilizowekwa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini pemba akielezea ushirikiano

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bandari Pemba, Abdallah Salum Abdallah, ametoa wito kwa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi ndani ya bandari hiyo kuimarisha ushirikiano na kutoa elimu kwa watendaji ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za bandari.

Sauti ya Mkurigezi wa bandari akitoa wito kwa taasisi

Naye Kamanda wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Pemba, Bakar Salum Othman pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Iptisam Fadhil, wameahidi kutoa ushirikiano na ushauri wa kitaalamu ili kuimarisha ulinzi na usimamizi wa shughuli za bandari hiyo.

Washiriki katika kikao kazi Bakar Salum Othman na Iptisam Fadhil