Micheweni FM
Micheweni FM
27 October 2026, 5:02 pm

Tasisi zisizo za kiserikali zina umhimu wa kuendeleza ushirikiano na Serikali ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Na Masanja Mabula.
MKUU wa Wilaya ya Wete, Abdalla Rashid Ali, amezitaka taasisi za kiraia kujenga utamaduni wa kurejesha faida kwa jamii kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo, hatua inayolenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada katika Hospitali ya Wilaya ya Kinyasini, Mkuu huyo wa Wilaya amesema taasisi za kiraia zina mchango mkubwa katika kuimarisha huduma za afya, hususan kwa akina mama wajawazito na watoto, hivyo ni muhimu kuendeleza ushirikiano na Serikali ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Mapema, Mkuu wa Kampuni ya Yas Zanzibar, Mohammed Waqid, amesema msaada huo uliotolewa katika hospitali hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Tumaini, inayolenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii, hususan sekta ya afya.
Msaada huo unatarajiwa kusaidia kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kinyasini, hususan kwa akina mama wajawazito na watoto