Micheweni FM

DC  Micheweni ahimiza upandaji Mikoko kukabiliana  mabadiliko tabianchi

4 November 2026, 3:10 pm

Pichani ni Mkuu wa Walaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja mwanzoni mwanzoni kushoto kwake niviongozi mbalimbali wanao tekeleza mradi wa Kijana Impact picha na Essau Kalukubila.

vijana mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya Pemba, amesema hatua hiyo inaonesha utayari wa vijana kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Na Essau Kalukubila.

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Khatib Juma Mjaja, amewataka wananchi kuongeza juhudi za kutunza mazingira kwa kupanda miti ya mikoko pembezoni mwa fukwe ili kuimarisha uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hususan katika maeneo yaliyoathiriwa na maji ya chumvi.

Mjaja ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji wa miti ya mikoko katika fukwe ya Tumbe, lililowakutanisha vijana mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya Pemba, amesema hatua hiyo inaonesha utayari wa vijana kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja

Aidha, Msimamizi  wa Mradi wa Kijana Impact, Hellen Sisya, amebainisha maeneo ambayo mradi huo unatekelezwa na kueleza kuwa lengo lake ni kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli za uhifadhi wa mazingira

Sauti ya Msimamizi  wa Mradi wa Kijana Impact, Hellen Sisya

Naye Mratibu wa Vijana kutoka ActionAid Tanzania Arif Fazel amesema ushiriki wa vijana katika miradi ya mazingira ni hatua muhimu katika kujenga jamii yenye uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda rasilimali za asili kwa vizazi vijavyo.

Sauti ya Arif Fazel Mratibu wa Vijana kutoka ActionAid Tanzania Arif Fazel

Kwa upande wao, wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wamepongeza juhudi za waandaaji na kuitaka jamii kuendelea kutunza mazingira kwa vitendo. Wamesema pamoja na kupanda miti, kuna haja ya kuhakikisha miti hiyo inalindwa na kuhudumiwa ili iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa

Sauti ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo