Micheweni FM

Mgogoro wa kiwanja Kizimbani wamfika RC mgeni

16 October 2026, 7:18 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya akiwa katika maeneo ya shehia ya Kizimbani wilaya ya Wete kwa lengo la kutatua mgogoro wa kiwanja Picha na Masanja Mabula

utatuzi wa mgogoro huo ili uweze kumalizika kwa amani na kuondoa tofauti zilizopo baina ya wananchi wanaohusika

Na Masanja Mabula.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, amewataka wananchi kuishi kwa upendo na mshikamano na kuachana na migogoro isiyokuwa na tija, akisisitiza kuwa maelewano na kuheshimiana ni nguzo muhimu katika kudumisha amani na kuleta maendeleo katika jamii.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo lenye mgogoro wa kiwanja katika Shehia ya Kizimbani, Mkuu huyo wa Mkoa amemtaka Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete, kusimamia kwa karibu utatuzi wa mgogoro huo ili uweze kumalizika kwa amani na kuondoa tofauti zilizopo baina ya wananchi wanaohusika.

Sauti ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya

Mapema, Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete, Shwena Hamad, alieleza kuhusu suala hilo na hatua zinazohusiana na utatuzi wa mgogoro huo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete, Shwena Hamad

Kwa upande wao, wananchi wanaohusika na mgogoro huo wameeleza kila mmoja chanzo cha mgogoro huo kwa mtazamo wake, wakibainisha mazingira yaliyopelekea kutokea kwa tofauti hizo katika eneo hilo.

Sauti ya wananchi wanaohusika na mgogoro huo

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amewahimza wananchi kutanguliza mazungumzo, kuheshimiana na kutumia njia za kisheria kutatua tofauti zao, kwani amani ndiyo msingi wa ustawi wa jamii na maendeleo endelevu.