Micheweni FM

Wizara ya Elimu Yahamasisha matumizi sahihi ya Mitandao ya Kijamii

26 November 2026, 2:47 pm

picha ya Mshauri wa Walimu wa Kituo cha Walimu Wilaya ya Wete, Bi. Mwajuma Mahadhi, akizungumuza katika kongamano la vijana lililo andaliwa na jumuiya ya vijana Pemba Picha na Essau Kalukubila.

Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa Walimu wa Kituo cha Walimu Wilaya ya Wete kilichopo Mitiulaya, Bi. Mwajuma Mahadhi, wakati akizungumza katika kongamano la vijana lililoandaliwa na Jumuiya ya Vijana Pemba ambalo limewakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Kisiwa cha Pemba.

Na Essau Kalukubila.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwapa wanafunzi elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kujiepusha na athari za matumizi mabaya ya mitandao hiyo.

Akizungumza katika kongamano la vijana lililoandaliwa na Jumuiya ya Vijana Pemba, Mshauri wa Walimu wa Kituo cha Walimu Wilaya ya Wete, Bi. Mwajuma Mahadhi, amesema kukua kwa teknolojia kunahitaji vijana kupewa elimu sahihi ili kuitumia mitandao ya kijamii kwa maendeleo yao na ya jamii.

Sauti ya Mshauri wa Walimu wa Kituo cha Walimu Wilaya ya Wete, Bi. Mwajuma Mahadhi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Said Mussa Rashid, amesema kongamano hilo limeandaliwa baada ya kubaini kupitia utafiti mdogo kuwa baadhi ya vijana wanatumia mitandao ya kijamii kinyume na maadili na malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Said Mussa Rashid

Washiriki wa kongamano hilo wameipongeza jumuiya hiyo kwa kuwapatia fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu, huku wakiahidi kutumia mitandao ya kijamii kwa njia chanya na kuwahamasisha vijana wenzao kufanya hivyo.

Sauti ya washiriki wa komgamano hilo.