Micheweni FM
Micheweni FM
17 September 2026, 12:45 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe Mgeni Khatib Yahya, amefanya ziara ya kushtukiza katika Shehia ya Utaani, ambapo amekagua hali ya usafi wa mazingira na kuwataka wananchi kuongeza juhudi katika kuhifadhi usafi wa maeneo yao ili kuepuka milipuko ya magonjwa na kujenga mazingira salama na yenye afya kwa jamii.
Na Mwiaba Kombo
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi, huku akiwataka viongozi wa Shehia kushirikiana na wananchi kuhakikisha taka zinakusanywa na maeneo ya makazi yanakuwa safi wakati wote.
Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abdalla Rashid Ali, pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete, Shuwena Hamad Ali, wamewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira, wakisisitiza kuwa usafi si jukumu la Serikali pekee bali ni wajibu wa kila mwananchi.
Nao baadhi ya wananchi wameahidi kudumisha usafi wa mazingira huku wakitoa wito kwa wananchi kushirikiana kuweka mazingira katika hali ya ya usalama.