Micheweni FM

Wanawake Pemba watakiwa kugombea nafasi za uongozi

7 July 2025, 7:42 pm

Katibu wa chama cha wananchi CUF taifa Husna Mohd Abdalla akizungumza na viongozi mbali mbali wa chama hicho katika ukumbi wa Sammail Gombani Pemba (picha Mwiaba Kombo)

Chama cha wananchi CUF ni miongoni mwa chama cha siasa ambacho kitashiriki uchaguzi mkuu Taifa ambao unatarajiwa kufanyika October 2025 ambapo viongozi wa chama hicho wamewataka wanachama wao pamoja na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi huo kwa kupiga kura ili kuweza kuwachagua viongozi ambao ni bora na watakao ongoza majimbo na taifa kwa ujumla .

Na Mwiaba Kombo

Chama cha  wananchi CUF Taifa kimewata kawatia nia katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kufahamu kuwa watakapopata ridhaa ya kugombea nafasi hizo kuwa wapo kwa ajili ya kuwatumikiawananchi.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa chama hicho Taifa Husna Mohd Abdalla wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa chama hicho ngazi ya Matawi , majimbo na Wilaya  huko katika ukumbi wa Samail Gombani Pemba amesema mwanasiasa yeyote ambae atagombea nafasi na kubahatika kuchaguliwa ajue kwamba amepata nafasi hio kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na sio chama chake.

Akizungumzia kuhusu wanawake amesema chama chake kitahakikisha kinawapa fursa wanawake nahawapati changamoto yoyote katika mchakato wa kugombania nafasi za uongozi.

Kwa upandewake  NaibuMkurugenzi wa habari kutoka chama cha  CUF  Ali  Rashid Abarani amewataka wachama ambao niwajumbe watakaoshiriki katika kuwapigia kura watiania kuwa niwajumbe  kutoka tawi husika ili atakaechaguliwa awe ni kutoka jimbo lililokusudiwa

Nae Mjumbe wa baraza kuu taifaHasina Mohammed Sharif  amewataka wanawake kujitokeza kuchukuafomu za kugombania nafasi mbalimbali za uongozi bila ya woga kwani wanachama wote wanahakisawa katika chama .

Mapema viongozi hao pamoja na wanachama wa chama hicho wamezindua tawi jipya machomanne Chake chake Pemba.