Micheweni FM

Bhangi yampeleka Masoud chuo cha mafunzo miaka saba

6 June 2025, 11:16 am

Picha ambayo ikimuonyesha Masoud Hamad Omar ambae amekutiwa hatian kwa kosa la kukamata na dawa za kulevya aina yabhangi yenye uzito wa gm 460 katika kijiji cha Sizini wilaya ya Micheweni Pemba (Picha na mtandao)

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar ni kosa kinyume na kifungu cha 23 (1) (a) (3) cha sheria nambari 8 ya mwaka 2021, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anafuata sheria ambazo zimewekwa

Na Fatma Hamad

Mahkama ya Mkoa Wete imempeleka Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka Saba (7) Masoud Hamad Omar mwenye umri (52) mkaazi wa Sizini Micheweni Pemba kwa shitaka la kupatikana na mafurushi Saba (7) ya dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa gm 460.
Kabla ya kusomwa huku mshitakiwa Masoud ameiomba Mahkama imfanyie shufaa wakati itakapompa adhabu kwani anafamilia zaidi ya watoto Watano inamtegemea.
Hakimu wa Mahkama hiyo ya Mkoa Zuwena Mohamed Abdul kadir amesema jumla ya mashahidi saba walisikilizwa mahkamani hapo, na Mahkama imeridhika na ushahidi uliotolewa dhidi yake juu ya shitaka la kupatikana na bhangi, hivyo atatumikia Chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka Saba (7) au kulipa faini ya shilingi Milioni 5,000,000.
Mapema mwendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka DPP Juma Mussa Omar alisema hana pingamizi na hukumu hiyo iliyotolewa, kwani wameshamaliza kuwasikiliza mashahidi wote na tayari walishafunga ushahidi juu ya shauri hilo.
Imedaiwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 4 mwaka huu majira ya saa 10 : zajioni katika kijiji cha Sizini bila ya halali na alipatikana na mafurushi hayo saba ya dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa gm 460.
Ikiwa kufanyahivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 23 (1) (a) (3) cha sheria nambari 8 ya mwaka 2021, Sheria ya kuanzishwa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar.