Micheweni FM

Waziri wa Kilimo ataka masharti ya mikopo yapunguzwe kwa wakulima, wafugaji

4 October 2026, 4:25 pm

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar akifungua mafunzo ya siku mbili yanayowakutanisha wakulima, wafugaji na wavuvi kutoka majimbo ya Kiwani na Mtambile Picha na Essau Kalukubila.

Waziri Suleiman amesema kuna haja ya taasisi za kifedha kuangalia upya vigezo vya utoaji wa mikopo ili kundI hilo muhimu katika uchumi liweze kunufaika na huduma za kifedha.

Na Masanja Mabula

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Suleiman Masoud Makame, amezitaka taasisi za kifedha kupunguza masharti ya mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, akisema masharti hayo yamekuwa kikwazo kwa wananchi hao kupata mitaji na kufikia malengo yao ya kiuchumi.

Akifungua mafunzo ya siku mbili yanayowakutanisha wakulima, wafugaji na wavuvi kutoka majimbo ya Kiwani na Mtambile yaliyoandaliwa na viongozi wa majimbo hayo, Waziri Suleiman amezitaka taasisi za kifedha kuangalia upya masharti ya mikopo, ili kuwawezesha kupata fursa za kifedha kwa urahisi zaidi

Sauti Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Suleiman Masoud Makame

Mbunge wa Jimbo la Kiwani Hija Hasan Hija pamoja na wawakilishi wa taasisi za kifedha wamesema wakulima, wafugaji na wavuvi wanapaswa kutumia majukwaa mbalimbali yanayotolewa na taasisi hizo ili waweze kunufaika na huduma za kifedha.

Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea washiriki ujuzi wa kilimo, ufugaji na uvuvi pamoja na kuwajengea uwezo katika masuala ya biashara na matumizi ya huduma za kifedha.