Micheweni FM

Mbunge awapiga jeki wakulima wa Mwani Kaskazini Pemba  

5 October 2026, 8:24 pm

Baadhi ya wakulimu wa zao la Mwani wa Mkoa wa Kaskazini pemba wakiwa katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na Mbunge viti maalum Mkoa huo Picha na Essau Kalukubila.

Wakulima hao wamesema changamoto hizo zimekuwa zikikwamisha uzalishaji wa mwani na kuathiri kipato

Na Masanja Mabula

Wakulima wa mwani Mkoa wa Kaskazini Pemba wamekutana na Mbunge wa Viti Maalum, Asha Omar Rashid, na kueleza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao, ikiwemo ukosefu wa mbegu bora na vifaa vya kilimo.

Wakulima hao wamesema changamoto hizo zimekuwa zikikwamisha uzalishaji wa mwani na kuathiri kipato chao, hivyo kuomba msaada wa kupata vifaa na mbegu bora zitakazowawezesha kuimarisha shughuli zao.

Sauti ya baadhi ya wakulima wa zao la mwani Kaskazini Pemba

Naye Mbunge huyo amewapatia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne, huku akiahidi kuwaunganisha na wataalamu watakaowawezesha kupata taaluma ya kusarifu mwani na kuongeza thamani ya mazao yao, sambamba na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Sauti ya Mbunge na Mwenyekiti wa UWT Kaskazini Pemba

Hatua hiyo ya Mbunge Asha Omar Rashid kuwasaidia vifaa inalenga kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na kipato, pamoja na kunufaika zaidi na shughuli ya kilimo cha mwani.