Micheweni FM
Micheweni FM
21 September 2026, 12:56 pm

Jumuiya ya Makada wa Afya Micheweni imewafariji na kuwapatia msaada akinamama wajawazito pamoja na waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwapa moyo na faraja katika kipindi hiki muhimu cha maisha yao.
Na Masanja Mabula
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Juma Mbwana Kombo, amesema lengo la kufika katika wodi ya akinamama wajawazito na waliojifungua ni kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa jamii ipo pamoja nao.
Amesema hatua hiyo inalenga kuonyesha mshikamano na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wahudumu wa afya katika kuhakikisha akinamama pamoja na watoto wao wanapata huduma zinazohitajika.
Nao uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni umeishukuru Jumuiya hiyo kwa kuguswa na hali ya akinamama wajawazito, waliojifungua pamoja na watoto wao na kuamua kuwafikia kwa kuwapa faraja na msaada.
Baadhi ya akinamama waliopokea msaada huo wameishukuru Jumuiya hiyo kwa kuwafariji na kuwapatia msaada, huku wakitoa pongezi kwa uongozi wa hospitali kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa akinamama wajawazito na waliojifungua pamoja na watoto wao.
Jumuiya hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni katika kuunga mkono juhudi za kuboresha afya na ustawi wa akinamama pamoja na watoto, hasa katika kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua