Micheweni FM

RC Kaskazini Pemba azindua siku ya unawaji mikono

16 October 2026, 6:44 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya akizindua siku ya unawaji wa mikono Mkoani humo Picha na Masanja Mabula.

viongozi wa jamii na viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usafi wa mikono.

Na Masanja Mabula

MAADHIMISHO ya Siku ya Kimataifa ya Kunawa Mikono yanayofanyika Oktoba 15 ya kila mwaka yamekuwa fursa ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kama njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Akizindua kampeni ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni,katika viwanja vya Maoneho Chamanangwe, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, amewaagiza viongozi wa jamii na viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usafi wa mikono.

Sauti ya  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya

Mapema, Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abdalla Rashid Ali, amesema kuwa kunawa mikono ni kinga muhimu dhidi ya maradhi, huku akihimiza wananchi kuzingatia utaratibu huo katika maisha yao ya kila siku.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abdalla Rashid Ali

Kwa upande wao, wataalamu wa afya wamesema kuwa unawaji sahihi wa mikono husaidia kuondoa vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa, yakiwemo kipindupindu na magonjwa ya kuhara, na hivyo kulinda afya za wananchi.

Sauti ya wataalamu wa afya wamesema kuwa unawaji sahihi wa mikono husaidia kuondoa vijidudu

Wamewataka wananchi kunawa mikono kabla ya kula, kabla ya kuandaa chakula na baada ya kutumia choo, wakisisitiza kuwa kuzingatia usafi wa mikono ni hatua rahisi lakini yenye manufaa makubwa katika kuzuia maambukizi na kujenga jamii yenye afya bora.