Micheweni FM

Jeshi la Polisi Kaskazini Pemba lachunguza kifo cha Mwanafunzi kidato cha kwanza

5 October 2026, 4:30 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ni SACP William Mwampaghale akizungumzia tukio la mwanafunzi wa kidato cha kwanzaRaiyan Hemed Amour kuuwawa Picha na Jeshi la Polisi

mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Raiyan Hemed Amour, mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa kijiji cha Kwale Mpona, shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, ambaye mwili wake ulikutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali

Na Essau Kalukubila.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Raiyan Hemed Amour, mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa kijiji cha Kwale Mpona, shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, ambaye mwili wake ulikutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, kabla ya tukio hilo, baba mzazi wa mtoto huyo alifika katika Kituo cha Polisi Wete usiku wa Oktoba 2, 2026 kutoa taarifa ya kupotea kwa mtoto wake, ambapo jalada la uchunguzi lilifunguliwa.

Sauti Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ni SACP William Mwampaghale

Aidha, Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za matukio ya kihalifu kupitia vituo vya polisi na kuacha kujichukulia sheria mikononi, huku likisisitiza kuwa linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwakamata waliohusika na tukio hilo.