Micheweni FM

Vijana wahimizwa kutumia teknolojia kwa usahihi

19 November 2026, 3:06 pm

Picha ya baadhi ya vijana wa Pemba wakiwa kwenye mafunzo ya siku moja yalio andaliwa na jumuya ya Vijana Pemba kaika ukumbi wa Kituo cha Mafunzo kwa Vijana Weni uliopo Wete Picha na Essau Kalukubila.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Masoud Mbaruku Haji, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa vijana yaliyofanyika katika Kituo cha Mafunzo kwa Vijana Weni, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Na Essau Kalukubila.

Vijana wa Pemba wametakiwa kuwa makini katika matumizi ya teknolojia na mitandao ya kijamii ili kuepuka vitendo vinavyoweza kuwafanya wajikute katika mikono ya sheria, badala yake kuitumia kama nyenzo ya kujiongezea maarifa, ujuzi na fursa za maendeleo.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Masoud Mbaruku Haji, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa vijana yaliyofanyika katika Kituo cha Mafunzo kwa Vijana Weni, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia kumeleta fursa nyingi kwa vijana, hivyo ni muhimu kuitumia kwa manufaa katika elimu, biashara na kujenga mustakabali bora wa maisha yao pamoja na kudumisha amani katika jamii.

Sauti ya Katibu wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Masoud Mbaruku Haji

Naye Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Faki Ali Faki, amesema changamoto kubwa inayowakabili baadhi ya vijana ni matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa kujifanya waandishi wa habari bila kufuata misingi na sheria za nchi, hali inayoweza kuwaingiza katika matatizo ya kisheria.

Amesisitiza umuhimu wa vijana kupata elimu sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuitumia kwa uwajibikaji na kwa manufaa ya jamii.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Faki Ali Faki

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Halima Haji Hamad na Omar Ali Faki, wameishukuru Jumuiya ya Vijana Pemba kwa kuandaa mafunzo hayo wakisema yamewasaidia kuelewa namna bora ya kutumia mitandao ya kijamii katika kutafuta fursa za maendeleo na kuchangia kuhifadhi amani nchini.

Sauti ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Halima Haji Hamad na Omar Ali Faki