Micheweni FM

RC Kaskazini Pemba aridhishwa na maandalizi ya maonesho siku ya Chakula

6 October 2026, 11:37 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgani Khatib Yahya akizungumza na katika kiwanja cha maonyesho ya chakula Chamanangwe Shehia ya Kiuyu Minungwini Wilaya ya Wete Mkoaha huo Picha na Essau Kalukubila

Maonesho ya Siku ya Chakula yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chamanangwe, huku akieleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya tukio hilo.

Na Masanja Mabula

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, ameongoza Kamati ya Usalama ya Mkoa huo kukagua maandalizi ya Maonesho ya Siku ya Chakula yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chamanangwe, huku akieleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya tukio hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukagua maandalizi hayo, Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka jamii kutumia fursa ya maonesho hayo kupata elimu na taaluma mbalimbali zinazohusiana na uzalishaji na matumizi bora ya chakula.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, amewataka vijana kutumia fursa hiyo kujifunza masuala ya kilimo biashara, kwa kutumia maarifa watakayoyapata katika kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji kwa ajili ya kujipatia kipato huku Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Idriss Hassan Abdalla akisema katika maonesho hayo wanarajia kusambaza mbegu za muhogo zilizofanyiwa utafiti

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na Afisa mdhamini Wizara ya Kilimo

Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa fursa kwa wananchi, hususan vijana, kupata elimu na maarifa kuhusu kilimo na kilimo biashara, huku wakitakiwa kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi na kukuza shughuli za uzalishaji.