Micheweni FM
Micheweni FM
12 October 2026, 8:27 pm

Makatibu wa matawi pamoja na sekretarieti za wadi na matawi wa Jimbo la Kiwani yenye lengo la kuwaimarisha katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya chama
Na Masanja Mabula.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Pemba kimesema hakitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwanachama yeyote katika Mkoa huo atakayebainika kuanza kupanga safu za uongozi kabla ya muda wa uchaguzi wa ndani ya chama uliopangwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa chama kuanzia ngazi ya mabalozi, makatibu wa matawi pamoja na sekretarieti za wadi na matawi wa Jimbo la Kiwani yenye lengo la kuwaimarisha katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya chama.
Kwa upande wao, wajumbe wa Mkutano huo, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kiwani, Hija Hassan Hija, wamewataka wanachama wa CCM kujiepusha na makundi ndani ya chama na badala yake kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano ili kulinda maslahi ya chama.