Micheweni FM
Micheweni FM
12 November 2026, 12:42 pm

Wakulima wa Mboga mboga na matunda wa kikundi cha Vumilia Maudhi wakionyesha kutoridhishwa na mweneno wa kilimo chao kinacho kabiliwa na changamoo ya maji paomja na magjwa ya mazao.
Na Essau Kalukubila.
Wakulima wa mbogamboga na matunda wa Shehia ya Chimba, Wilaya ya Micheweni, wameiomba Serikali kuwatazama kwa jicho la huruma kwa kuwapatia ufumbuzi wa changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiathiri shughuli zao za kilimo kwa muda mrefu sasa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la Kwamema, Chimba, mwenyekiti wa kikundi cha Vumilia Maudhi, Rashid Khatib Rashid, amesema kuwa pamoja na juhudi kubwa wanazozifanya katika uzalishaji wa mazao mbalimbali, bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa maji unaokwamisha maendeleo ya kilimo chao.
Kwa upande wake, Katibu wa kikundi hicho, Sharafu Salum Khamad, ameeleza kuwa wakulima hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya umwagiliaji wa mazao yao, hali inayoongeza gharama na kupunguza ufanisi wa uzalishaji. Ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi na wadau wa maendeleo kusaidia kutatua tatizo hilo ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa kikundi cha Vumilia Maudhi, Omar Hamad Seif, amesema kuwa licha ya kuendelea kujishughulisha na kilimo cha matunda hususan mananasi, bado wanakabiliwa na upungufu wa elimu ya kisasa ya kilimo hicho. Amesema hali hiyo husababisha mazao kushambuliwa na magonjwa mbalimbali huku wakishindwa kupata njia sahihi za kuyadhibiti.
Wakulima hao wameeleza matumaini yao kuwa serikali pamoja na taasisi zinazohusika na maendeleo ya kilimo zitachukua hatua za haraka kuwasaidia kupata huduma ya maji pamoja na mafunzo ya kitaalamu yatakayochangia kuongeza uzalishaji, kuimarisha kipato chao na kukuza uchumi wa jamii ya Chimba na eneo la Micheweni kwa ujumla.


