Micheweni FM
Micheweni FM
7 October 2026, 3:56 pm

Changamoto zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara na kuimarisha usalama wa wanafunzi wanaotumia njia hizo kwenda na kurejea skuli.
Na Essau Kalukubila.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara na kuimarisha usalama wa wanafunzi wanaotumia njia hizo kwenda na kurejea skuli.
Ahadi hiyo ameitoa wakati wa ziara yake kijijini hapo, ambapo alikagua njia zinazotumiwa na wanafunzi pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi kufuatia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi Raian Hemed akiwa njiani kurejea nyumbani kutoka skuli.
Kwa upande wao, wananchi wameiomba Serikali kuongeza juhudi katika kuboresha njia za mawasiliano zinazotumiwa na wanafunzi, huku wakisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na jamii ili kuhakikisha usalama wa watoto wanapokwenda na kurejea skuli.
Hataivyo nae Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Nestory Didi ametoa wito wa kuwataka kujisalimisha mapema wale walio husika na tukio la mauwaji ya Mwanafunzi wa Kijiji hicho akibainisha msako wa kuwabaini umeanza

Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Nestory Didi akizungumza katika mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba katika kijiji cha Kwale Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete kufuatia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi Raian Hemed akiwa njiani kurejea nyumbani kutoka skuli