Micheweni FM
Micheweni FM
3 November 2026, 5:53 pm

Vijana wamehimizwa kuzitambua fursa ili ziweze kuwapatia kipato nakuacha kuwa tegemezi kwa jamii.
Na Essau Kalukubila.
Waziri wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji Zanzibar Ali Suleman Ameir (Mrembo) amewata vijana kujiendelea katika fani mbalimbali ambazo zitapelekea kuwa na sifa za kuajirika katika taasisi za serikali na sekta binafsi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumuza na mabaraza ya vijana wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha WIAC na kuwataka vijana hao kuzitambua fursa hizo ili ziweze kuwapatia kipato.
Sambamba na hayo, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji Zanzibar, Seif Kombo Pandu, amesema dhamana aliyopewa na Rais wa Zanzibar ni kuhakikisha anashirikiana na wizara kutafuta fursa za kazi na ajira ili vijana wengi zaidi waweze kuajirika na hivyo kutimiza malengo ya wizara hiyo.
Kwa upande wao, vijana wa Wilaya ya Wete wamepongeza jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kiuchumi. Wamesema wameamua kujikwamua na umasikini kwa kuanzisha vikundi mbalimbali vya uzalishaji na ujasiriamali ili kuweza kusonga mbele zaidi kimaendeleo.