Micheweni FM

Waziri Haroun asisitiza utayali wakukabilinana na El Nino 

9 October 2026, 4:00 pm

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman Picha na Fatma Mohamed Salum

 kikao maalumu kilichoandaliwa na Afisi ya Mkoa ikiwa ni miongoni mwa mikakati iliyojipangia na kuwashirikisha viongozi wa vyama siasa wakiwemo  na watendaji wa manispaa  za wilaya kati na kusini, pamoja  na wataalamu kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.

Na Fatma Mohamed Salum

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman, amewataka viongozi wa Serikali na vyama vya siasa nchini kuendelea kuelimisha jamii kuhusu athari za mvua za El Nino na hatua za kuchukua ili waweze kukabiliana nazo.

Amesema kutokana na utabiri unaoendelea kutolewa na mamlaka ya hali ya hewa kwamba kiwango cha mvua  kilichotabiriwa kunyesha kwa mwaka huu ni kikubwa na haijawahi kutokea nchini hivyo suala hilo linahitaji nguvu za ziada na ushirikiano mkubwa katika kuwaelimisha wananchi ili wachukue tahadhari  za mapema.

Sauti ya Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mkoa huo, Mhe. Hamida Mussa Khamis, amesema kwa sasa  mpango mkakati wa Mkoa ni kuendelea kuhamasisha wananchi kupitia makundi mbalimbali ili kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha na kuchukua tahadhari za mapema kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Nino.

Sauti ya Mkoa wa Kusini Unguja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mkoa huo, Mhe. Hamida Mussa Khamis

Kwa upande wao washiriki katika kikao hicho wameiomba mamlaka ya hali ya hewa kuongeza juhudi za kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusiana na mvua hizo pamoja na taasisi nyengine ikiwemo ZECO ili kunusuru kutokea majanga kwani suala hili ni mtambuka na linapaswa kuekewa mikakati ya pamoja.

Sauti yawashiriki katika kikao hicho