Micheweni FM

Maonyesho siku ya chakula duniani yafungwa Chamanangwe

18 October 2026, 3:06 pm

Baadhi ya mwenekano viwanja vya maonyesho ya siku ya chakula Duniani yaliopo maeneo ya Chamenangwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini pemba Picha na Essau Kalukubila.

Agizo la Serikali la kulitumia eneo hilo kama kitovu cha kutoa cha  taaluma kwa wakulima na wafugaji, badala ya kusubiri kipindi cha maoneshagizo la Serikali la kulitumia eneo hilo kama kitovu cha kutoa cha  taaluma kwa wakulima na wafugaji, badala ya kusubiri kipindi cha maoneshoo

Na Masanja Mabula.

MAONESHO ya Siku ya Chakula yaliyokuwa yanafanyika katika viwanja vya Chamanangwe Kisiwani Pemba yametajwa kuwa jukwaa muhimu la kujifunza taaluma na ujuzi wa kilimo na ufugaji, kwa lengo la kuwawezesha wakulima na wafugaji kuongeza tija katika shughuli zao.

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo  Dkt. Hamad Omar Bakar akifunga maonesho hayo amewataka wakuu wa taasisi husika kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kulitumia eneo hilo kama kitovu cha kutoa cha  taaluma kwa wakulima na wafugaji, badala ya kusubiri kipindi cha maonesho.

Sauti ya Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo  Dkt. Hamad Omar Bakar

Afisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Idriss Hassan Abdalla, amesema wizara hiyo inaendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya kuimarisha kilimo na ufugaji wa kibiashara.

Sauti ya Afisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Idriss Hassan Abdalla

Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wakulima na wafugaji kujifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji, kupata teknolojia mpya na kuongeza uzalishaji, kipato pamoja na kuimarisha usalama wa chakula.