Micheweni FM

Mkuu wa Wilaya ya Chakechake awatia Moyo Wanafunzi wa kidato cha pili

8 October 2026, 8:36 pm

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Zuhura Mgeni Ohuman akizungumza na mmoja wa wanafunzi katika Skuli ya Sekondari Madungu Picha na Essau Kalukubila.

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Zuhura Mgeni Ohuman, amewataka wanafunzi wa kidato cha pili katika Skuli ya Madungu kuongeza bidii katika masomo yao na kujiandaa vyema kwa mtihani wa taifa unaotarajiwa kuanza Oktoba 12 mwaka huu.

Na Essau Kalukubila.

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Zuhura Mgeni Ohuman, amefanya ziara katika Skuli ya Madungu na kuwataka wanafunzi wa kidato cha pili kufanya maandalizi ya mwisho kwa umakini ili kufanya vizuri katika mtihani wa taifa unaotarajiwa kuanza Oktoba 12 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa ziara  katika Skuli hiyo, mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa elimu ni msingi muhimu wa maendeleo ya mwanafunzi na taifa kwa ujumla, hivyo amewahimiza wanafunzi kutumia muda uliobaki kufanya marudio ya masomo yao na kuzingatia maelekezo ya walimu.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Madungu Rashid Mzee amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutembelea skuli hiyo, akieleza kuwa ziara hiyo imewapa hamasa kubwa walimu na wanafunzi, hasa wale wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Madungu Rashid Mzee

Kwa upande wao, wanafunzi wa skuli hiyo wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao, wakisema wamejipanga kwa kutumia maarifa na miongozo waliyopewa na walimu wao katika kipindi chote cha masomo.