Micheweni FM
Micheweni FM
11 November 2026, 3:57 pm

Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, alipoyefika ofisini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo
Na Mwandishi Wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Hamida Mussa Khamis, amesema uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji unaendelea kufungua fursa za uwekezaji, biashara na kukuza uchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Tunguu, wakati akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, alipoyefika ofisini kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Mhe. Hamida amesema ziara hiyo ni fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uchumi, ikiwemo kilimo cha mwani, ambacho ni miongoni mwa shughuli zenye mchango mkubwa katika uchumi wa Zanzibar.
Amesema Mkoa wa Kusini Unguja una fursa mbalimbali za kiuchumi, hivyo ushirikiano huo unaweza kusaidia kuvutia wawekezaji, kupanua masoko na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa na wananchi.
Kwa upande wake, Balozi wa Msumbiji Ricardo Mtumbida amesema ziara hiyo inalenga kujifunza uzoefu kupitia Mkoa wa Kusini Unguja katika masuala ya biashara na uchumi, hususankilimo cha mwani, ili kuona namna nchi hizo zinavyoweza kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wake.