Micheweni FM
Micheweni FM
3 October 2026, 3:24 pm

mkutano wa kupokea ripoti ya utafiti kuhusu matumizi ya vyoo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, uliowasilishwa na taasisi ya OIKOS
Na Essau Kalukubila.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya amehimiza wananchi kutumia vyoo kwa usahihi na kuzingatia usafi wa mazingira, akibainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuzuia magonjwa na kulinda afya ya jamii.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano wa kupokea ripoti ya utafiti kuhusu matumizi ya vyoo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyowasilishwa na taasisi ya Oikos.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Khatib Juma Mjaja, pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete, Shuwena Hamad Ali, wamesema matumizi sahihi ya vyoo na usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi.
Kwa upande wao watendaji wa taasisi ya OIKOS wamesema utafiti umebaini kuwepo kwa changamoto katika matumizi sahihi ya vyoo katika wilaya ya Wete na Micheweni.
Lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kila mwananchi anatumia choo kwa usahihi, anazingatia usafi, na hivyo kuchangia kujenga jamii yenye afya na mazingira salama.