Micheweni FM
Micheweni FM
14 November 2026, 7:37 am

Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni wametakiwa kusimamia ipasavyo vyanzo vya mapato vilivyopo katika wilaya hiyo ili kuhakikisha halmashauri inakusanya mapato kwa kiwango kilichokusudiwa.
Na Mwiaba Kombo
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Khatib Juma Mjaja, wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni.
Aidha, amesema kuwa ushirikiano kati ya watendaji na madiwani ni jambo muhimu katika kuhakikisha vyanzo vya mapato vinasimamiwa vizuri na mapato yanakusanywa kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Masoud Ali Hamad, amesema kuwa dhamira ya kuchaguliwa kuwa madiwani ni kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata maendeleo kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali huku mkurugenzi Hamad Khatib Saleh, amewataka madiwani kuendelea kushirikiana na watendaji katika kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha yanatumika katika kuwaletea wananchi maendeleo.