Micheweni FM
Micheweni FM
3 November 2026, 6:15 pm

waumini kuheshimu mamlaka zilizopo na kufuata taratibu na sheria zilizowekwa, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda umoja, kuimarisha mahusiano na kuhakikisha jamii inaendelea kuishi
Na Essau kalukubila.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Askofu Lameck Ndomba, amewataka waumini wa kanisa hilo kuepuka kuwa chanzo cha migogoro katika jamii inayowazunguka pamoja na Serikali, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, upendo na mshikamano.
Akizungumza wakati wa misa iliyofanyika katika kanisa hilo eneo la Kizimbani, Wete, Askofu Ndomba amewataka waumini kuheshimu mamlaka zilizopo na kufuata taratibu na sheria zilizowekwa, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda umoja, kuimarisha mahusiano na kuhakikisha jamii inaendelea kuishi kwa amani na maelewano.
Naye Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, George Etieno, amelitaka kanisa hilo upande wa Pemba kuanzisha miradi ya maendeleo itakayosaidia kuboresha maisha ya waumini na jamii kwa ujumla, huku akisisitiza umuhimu wa kanisa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na ustawi wa wananchi.
Wito huo unalenga kuimarisha nafasi ya kanisa katika kudumisha amani, mshikamano na kuchochea maendeleo ya kijamii.