Micheweni FM

RC Mgeni amezipongeza juhudi za viongozi wa Dini  kusimamia Amani

31 October 2026, 3:33 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu wa Kanisa Anglikana Zanzibar, Lameck Ndomba Picha na Masanja Mabula.

katika kudumisha amani ya nchi, hivyo ni muhimu kuendelea kutumia majukwaa yao kuhimiza wananchi kuishi kwa upendo na mshikamano.

Na Masanja Mabula.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya, amezipongeza juhudi za viongozi wa dini katika kusimamia amani na mshikamano wa taifa, akiwataka kuendeleza jukumu hilo muhimu kwa kuhubiri upendo, umoja na utulivu miongoni mwa wananchi.

Akizungumza na uongozi wa Kanisa la Anglikana Zanzibar uliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kudumisha amani ya nchi, hivyo ni muhimu kuendelea kutumia majukwaa yao kuhimiza wananchi kuishi kwa upendo na mshikamano.

Sauti ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mgeni Khatib Yahya,

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Lameck Ndomba, ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza huduma mbalimbali za kijamii zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar, Lameck Ndomba na Katibu wa Kanisa la Anglikana Zanzibar

Viongozi wa Serikali wameendelea kulitaka Kanisa hilo kuwa karibu na Serikali kwa kushirikiana katika shughuli za maendeleo na huduma za kijamii ili kuimarisha ustawi wa wananchi.

Sauti ya Viongozi wa Serikali wameendelea kulitaka Kanisa hilo kuwa karibu na Serikali

Ziara hiyo inatajwa kuwa muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini katika kujenga jamii yenye amani, upendo, mshikamano na maendeleo endelevu.