Wenye ualbino wahakikishiwa ulinzi na jeshi la polisi Mwanza
24 May 2024, 8:09 pm
Licha ya jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu na kukemea vitendo vya uhalifu nchini baado lindi la biasharra za viungo vya binadamu hasa wenye ulemavu wa Ngozi linaaendelea kutokea hasa kwa mikoa ya kanda ya Ziwa.
Na;Emmanuel Twimanye
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limewagiza maafisa watendaji wa kata Wilayani Sengerema kuanzisha ulinzi shirikishi katika kata zao ili kuimarisha ulinzi dhidi ya watu wenye ualbino.
Agizo hilo limetolewa na Mratibu wa Polisi jamii Mkoa wa Mwanza Jovitha Tibangayuka kwa niaba ya Kamanda wa polisi Mkoani mwanza Wilbroad Mtafungwa katika kikao cha kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi dhidi ya watu wenye ualbino kilichofanyika Wilayani Sengerema, huku akikemea waganga wa tiba asili wanaopiga ramli chonganishi .
Baadhi ya maafisa watendaji wa kata wamelipongeza jeshi la polisi kwa mikakati hiyo na kuahidi kwenda kutekeleza suala hilo ili kuimarisha ulinzi wa kundi hilo.
Nao baadhi ya watu wenye albinism wameiomba serikali kuendelea kuimarisha ulinzi dhidi yao ili kunusuru maisha yao.
Aidha hivi karibuni mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka 10 anayesoma Darasa la nne shule ya msingi maalumu Katoro Mkoani Geita amenusurika kifo baada ya kudaiwa kushambuliwa na mtu asiyefahamika kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwa na mkono .