Waziri wa ardhi azindua baraza la Ardhi Sengerema.
22 March 2022, 4:14 pm
Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya makazi Mh, Agelina Mabula amewataka watumishi wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya Wilaya nchini kutimiza wajibu wao kwa weledi kwa kuzingatia sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo iliyopo na itakayotolewa ili kuboresha utoaji wa huduma na utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua baraza la ardhi la wilaya ya Sengerema wilayani humo ambapo amesema kuwa mamlaka za nidhamu hazitasita kuwachukuliahatua za kinidhamu watumishi wanaoidharirisha serikali kwa kuendekeza viutendo vya rushwa.
Katika hatua nyingine Waziri huyo amewaonya wananchi wanaokimbilia katika maeneo ya uwezekaji kununua viwanja kwa lengo la kulipwa fidia na kusema kuwa hakuna mtu yeyote atakayelipwa fidia .
Nao baadhi ya wananchi Wilayani humo wamemshukru waziri huyo kwa kuzindua baraza la ardhi kwa kuwa uwepo wa baraza hilo wilayani Sengerema imewasaidia kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu wa kwenda Mkoa jirani wa Geita kufuata huduma za ardhi katika baraza la ardhi la mkoa huo.
Uzinduzi huu umehudhuliwa na viongozo mabalimbali wakiwemo viongozi wa chama cha mapinduzi CCm