TBS yatakiwa kufanya ukaguzi wa Bidhaa feki Mjini Sengerema.
5 May 2021, 5:05 pm
Shirirka la viwango nchina Tanzania TBS limetoa mafunzo ya usindikaji bidha za mchele kwa wajasilia mali Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Akizungumza baada ya kufungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa wilaya hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya Bwn. Alan augostine Mhina amewataka TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa wilayani Sengerema kwani kumekuwepo na baadhi ya wafanya biashara wanaouza bidhaa zisizo na ubora.
Kwa upande wake meneja wa mafunzo na utafiti (RTMM) Mwl.Hamis Sudi Mwanasala kwa niaba ya mkurungenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania TBS, amesema jambo hilo watalifanyia kazi la kuongeza wataalamu watakao kuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara wilayani hapo.
Naye Manager wa TBS Kanda ya ziwa Bwn,Ismail Joseph Mwaipaja amesema wameanda mafunzo haya maalumu kwa wajasiliamali wa bidhaa za mchele ili kuwawezesha namna ya kusindika na kufungasha bidhaa hizo.
Shirika la viwango Tanzania limeanza kutoa mafunzo ya ujasilia mali na usindikaji wa bidhaa za mchele kwa kushirikiana na mamlaka zingine kama SIDO pamoja na ofisi za halmashauri husika.