Huduma za Mawasiliano za zidi kuimalika Sengerema
15 January 2025, 4:34 pm
Sengerema ni miongoni mwa Halmashauri zilizonufaika na mradi wa ujenzi minara ya mawasiliano 758 nchini, ambapo minara miwili imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi Sengerema.
Na;Elisha Magege
Jamii imetakiwa kutunza na kuilinda miundombinu ya mawasiliano inayoendelea kujengwa ili kuimalisha huduma za mawasiliano nchini.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi baada ya kuutembelea mnara mpya wa simu za mkononi uliojengwa kijiji cha Sotta kata ya Igalula Wilayani Sengerema, Ambapo amesema serkali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa minara 758 nchi nzima na halmashauri ya Sengerema tayali minara miwili inafanya kazi kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga amemshukuru Mh. Rais wa jamhuri ya Muungani Dr.Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuimalisha miundo mbinu ya mawasiliano hasa eneo la kata ya Igalula ambako wanatarajia kuwa eneo lenye watu wengi kutokana na kuwepo kwa mgodi wa dhahabu wa Sotta Mining Ltd.
Wakizungumza kwa niaba ya Wanchi wa Sengerema Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh. Hamis Tabasam na Diwani wa Kata ya Igalula Sanije Shibiliti wameomba kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kupeleka minara na maeneo mengine yenye changamoto ili kuwasaidia wananchi kupata mawasiliano.
May 13 2023 rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan alizindua mradi wa ujenzi wa minara 758 nchini,ambapo minara miwili tayari imeshaanza kutoa huduma kwa wananchi wa kisiwa cha Lyakanyasi kata ya Chinfufu na kijiji cha Sotta kata ya Igalula Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.