Sengerema imepanda miti 500 kumbuukumbu ya miaka 63 ya uhuru
9 December 2024, 2:42 pm
Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 kutoka kwa mkoloni mwingereza, ikikabbidhiwa kwa mwl. julius K.Nyerere akiwa kama waziri mkuu wa kwanza mtanganyika na badae rais wa kwanza wa taifa hilo,na leo imetimia miaka 63 tangu kupatikana kwa uhuru huo.
Na;;Elisha Magege
Halmashauri ya Sengerema imeadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kupanda miti na kufanya usafi maeneo mbalimbali ya kijamii.
Akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Sekondari mpya Isungang’holo Katibu tawala wilaya ya Sengerema Curthbert Midala, amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupanda miti kwani inafaida nyingi ikiwemo kutunza mazingira.
Kwa upande wake Afsa mazingira Halmashauri ya Sengerema Bi.Tandy Laizer amesema jumla ya miti 500 imepandwa katika eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari isungang’holo ikiwemo miti ya matunda,mbao na vivulli.
Naye Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Bwn. Wilbert Bandola amewashukuru wananchi kujitokeza kuazimisha miaka 63 ya uhuru kwa kupanda miti eneo hilo.
Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isungang’holo Bwn.Michael Sumuni pamoja na wananchi wamewashukuru viongozi wa halmashauri ya Sengerema kwa kuteua eneo hilo kupanda miti huku wakiahadi kuitunza.
Hata hivyo wakala wa huduma za misitu Tanzaniaa (TFS) wilaya ya Sengerema inatoa miche ya miti bure kwa wananchi, lengo likiwa ni kupanda miti kwa kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.