Sengerema FM

Kijana ajikuta mikononi mwa polisi kwa kutaka kuoa kwa njia ya udaganyifu

13 November 2024, 9:11 pm

Kijana Poul Madege Bulima akiwa chini ya ulinzi ofisi za polisi jamii Mission Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye

Kijana mmoja aliye jitosa kutaka kuoa amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukosa mahali na kutaka kumraghai binti amutoroshe, nje na makubaliano na wazazi wake.

Na;Emmanuel Twimanye

Kijana anayedaiwa kufanya ulaghai wa kumuoa binti kwa njia ya udaganyifu katika kitongoji cha kizugwangoma  amekamatwa na Polisi jamii kata ya Misheni Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, huku mshenga wake  akitokomea kusikojulikana .

Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa binti aliyefanyiwa ulaghai na kijana huyo  amesema kuwa alifika nyumbani kwake akiwa na mshenga  na kujitambulisha kuwa  anahitaji kumuoa binti yake kisha  kukubaliana mahali, na ilipofika siku ya  kupeleka mahali  hawakuonekana  huku wakiisababishia hasara kubwa  familia ya mandalizi ya sherehe ndipo mama huyo alipobaini kuwa vijana hao walikuwa matepeli.

Sauti ya Bi.Tatu Kapaya Ngaka mama mzazi wa binti aliyetaka kuolewa

Binti aliyefanyiwa ulaghai na vijana hao amesema kuwa baada ya kutokea hali hiyo aliamua kuweka mtego ili kuwakamata vijana hao kwa kushilikiana na polisi jamii kata ya Misheni.

Sauti ya Binti Sikujua james aliye taka kulaghaiwa na vijana kuolewa

Kijana anayedaiwa kufanya ulagghai kwa binti huyo amekiri kuwa hakuwa na lengo la kuoa bali  alikuwa ni tapeli  huku akiomba msamaha kwa wazazi wa binti .

Sauti ya kijana muoaji

Baadhi ya  wananchi  na ndugu wa famili hiyo wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba serikali kumchukulia hatua kali za kisheria kijana huyo kwa  kitendo cha kumdharirisha binti huyo na kuisababishia familia ya binti hasara .

Sauti za wananchi na ndugu wa familia ya binti aliyetaka kuolewa

Askari wa polisi jamii  katika kata hiyo  Deogratius kaswahili  akieleza namna walivyo mkamata kijana huyo.

Sauti ya Askari wa polisi jamii  kata ya Mission  Deogratius kaswahili akizungumzia walivyomunasa kijana akijaribu kumlaghai binti kkumuoa

Naye kamanda mkuu wa polisi jamii kata ya Misheni Rajabu Tunge amethibitisha kukamatwa kwa kijana huo huku akisema kuwa kijana huyo atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku akiwataka vijana kuacha   utapeli.

Sauti ya kamanda mkuu wa polisi jamii kata ya Misheni Rajabu Tunge akizungumzia tukio hilo namna lilivyotokea