Sengerema FM

FDC Sengerema yakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia

6 November 2024, 11:34 am

Mkuu wa chuo cha maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) Bi.Monika Rukeha akisoma risala ya chuo kwa mgeni Rasmi.Picha na Joyce Rollingstone

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) kilianzishwa Mwaka 1978 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kupata ujuzi wa fani mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.

Na;Joyce Rollingstone

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC kilichopo Wilayani Sengerema,kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemi ukosefu wa Mashine yenye uwezo wa kushona viatu aina zote.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo hicho  Bi Monika Rukeha,wakati akisoma risala ya chuo mbele ya Mgeni Rasimi na kusema kuwa chuo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa mashine ya kushonea bidhaa za ngozi huku akitaja mafanikio yaliyofikiwa na chuo hicho.

Sauti ya mkuu wa chuo hicho  Bi Monika Rukeha akizungumzia upungufu wa vifaa vya kufundishia chuoni hapo

Aidha bi Rukeha hakusita kuwaasa wahitimu wa chuo hicho kutumia ufundi walioupata katika chuo hicho, na kuwaomba kufanya kazi kwa bidii na nidhamu.

Sauti ya mkuu wa chuo hicho  Bi Monika Rukeha akiwaasa wahitimu kutumia vyema taaluma yao
Mgeni rasimi Bwn,Japhet Samwel Kiboya akizungumza na wanafunzi wahitimu wa chuo cha maendeleo ya wannchi Sengerema

Naye Mgeni Rasimi  Bwan, Japhet Samwel Kiboya,ameanza kwa kuwashukuru wahitimu na kuwatia moyo kwa kuweza kukabiliana na mapungufu yaliyopo hapo chuoni ,na kuweza kukabiliyana nayo,na kuwaomba wakatumie vizuri ufundi walioupata chuoni na si kukaa kusubili ajira.

Sauti ya Mgeni Rasimi  Bwan, Japhet Samwel Kiboya akiwatia moyo wanafunzi na wahitimu chuo cha FDC

Nao wazazi waliohudhulia katika mahafari hiyo wamewapongeza walimu kwa kazi nzuri, pamoja na kutoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto kwenda kutumia ujuzi walioupata na si kukaa nyumbani na kusubili ajira,bali wajiajiri wakiwa wanasubili ajira.

Sauti za wazazi wa wanafunzi wa chuo cha FDC Sengerema

Hata hivyo  Mgeni Rasimi amepata flusa ya kuwatunuku vyeti wahitimu 229 wakike 57 na wakiume 172 kwa fani mbalimbali katika mahafali ya 25 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na na viongozi wa chama na serikali,pamoja na wazazi.