Sengerema FM

Vyombo vya habari vyatakiwa kufuata sheria kuandaa maudhui ya uchaguzi

29 October 2024, 9:08 am

Meneja huduma za utangazaji TCRA Eng.Andrew Kisaka akizungumzia kuhusu miongozo ya uchaguzi

Serikali na wadau wameendelea kutoa elimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, huku wananchi wakitakiwa kujitokeza kuchagua viongozi watakao wafaa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Na;Elisha Magege

Vyombo vya Habari nchini vimatakiwa kufuata sheria, kanuni na miongozi ya uchaguzi ili kuriport na kufanya vipindi bora vinavyo husu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Rai hiyo imetolewa na Mhandisi Endrew Kisaka Meneja wa huduma za utangazaji TCRA Kwenye mafunzo ya wandishi wa habari wandamizi inayofanyika Kibaha mkoani Pwani juu ya namna ya kuandaa maudhui yanayo husu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Sauti ya Mhandisi Endrew Kisaka Meneja wa huduma za utangazaji TCRA akifafanua sheria na kanuni za uchaguzi

Naye mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano TAMISEMI Bi.Nteghenjwa Hoseah amesema uchanguzi wa mwaka huu kila mgombea atapigiwa kura na wananchi hata akiwa mgombea pekee,na kwamba wananchi wajitokeza kuchagua viongozi watakao waongoza kwa kipindi cha miaka 5 ijayo kwenye mitaa,vijiji na vitongoji vyao.

Sauti ya mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano TAMISEMI Bi.Nteghenjwa Hoseah akizungumzia kanuni za uchaguzi serikali za mitaa 2024

Mafunzo haya yameandaliwa na chuo kikuu cha Dar es salaam shule ya uandishi wa Habari  na mawasiliano kwa Umma (SJMC) kupitia program ya Year book 2024 yenye lengo la kuwajengea uwezo wandishi wa Habari na   namna ya kuandaa maudhui bora yanayo husu uchaguzi serikali za mitaa 2024.