Vijana watakiwa kuchangamkia nafasi za uongozi serikali za mitaa
28 October 2024, 10:48 am
Vijana wengi nchini wamekuwa na tabia ya kuacha kuomba nafasi za uongozi ngazi za serikali za mitaa jambo linalo tajwa kurudisha nyuma maendeleo ya vijiji na mitaa nchini.
Na;Elisha Magege
Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kugombea uongozi uchaguzi serkali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa na kijana mzalendo Sir.Muron Mwita katika mahojiano maalumu na Radio Sengerema ambapo amesema kumekuwepo na kasumba ya vijana kutokuchangamkia nafasi za uongozi ngazi za mitaa na vijiji huku wakiamini ni kazi za wazee.
Katika hatua nyingine Sir.Mwita amesema vijana wanatakiwa kuungana na kushirikiana kutatua changamoto zilipo kwenye jamii huku akiwataka vijana kuwekeza katika elimu pia wajitokeza bila kuogopa walioko mbele walivyo na nguvu kiuchumi.
Aidha Diwani wa kata ya Tabaruka Mh. Sospiter Simon Busumabhu amesema vijana wakiamua wanaweza huku akitoa mfano yeye alivyoweza kupata nafasi ya uongozi akiwa kijana mdogo na masikini.
Hata hivyo Sir.Mwita amesema kuwa Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi, hivyo ni wakati wa vijana kutambua fursa za vyama vilivyopo nchini.