Tabasamu ashirikiana na wananchi kujenga daraja
15 October 2024, 6:48 pm
Wananchi wa kijiji cha Butonga wilayani Sengerema wafurahia serkali ya awamu ya sita chini ya Dr.Samia kwa kuanza ujenzi wa daraja lililokuwa likisababisha vifo kwao kwa muda mrefu.
Na;Emmanuel Twimanye
Daraja lililokuwa likihatarisha maisha ya wananchi katika Kijiji cha Butonga kata ya Igulumuki Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza limeanza kujengwa na Serikali ili kunusuru maisha ya wakazi wa Kijiji hicho.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Sengerema kwa kusimamia ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa litakapokamilika litawasaidia kuokoa maisha ya wananachi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam ameridhiwa na ujenzi wa daraja hilo pamoja na ujenzi wa barabara ya yenye urefu wa Kilomita 53 kutoka Sengerema hadi mizolozolo na kuipongeza serikali kwa ujenzi huo .
Ujenzi wa daraja hilo linagharimu kiasi cha Tsh.180 na unatarajia kukamilika mwezi November 30 mwaka huu.